ACKNOWLEGMENT


Dear Friends and Relatives
First of all I would like to tahanks Almighty God the creator of everything, he blessed me with the faculty of understanding, physical and spiritual strength to accomplish my college studies.

I acknowledge the presence, prayers and heartily financially assistance of my Parents Mr. and Mrs. Mathias Mwaminifu, my brother Laurent,Bernard and my sister Gaudencia who they comforted me much when I was tired and their encouragement may God bless you all.
I would also like to thank the management of IAA and my classmates for the time we used together which increase my knowledge in IT related environment, also it has really been a rewarding experience in working environment at large, be blessed all.
I won’t be fair if I won’t express my gratitude to my X-Co-workers at Resolute,Mr. Shiwala, Henry, Lubimbi,DonnyP,Mzee Mwenzangu Dotto, Albert, Sylver, ManFas, Yohana, and my supervisors Mwanjoka and Zac for your challeges and supports. classmates Inno, Ekson,peninna,lily,Elisha,Viji,Jachi, and Reny.
It’s not easy to mention each and everyone by name. God bless you all.
TUNAADHIMISHA SIKU YA MWALIMU NYERERE LEO
Mwalimu akiwa Butiama
Kaburi la Mwalimu Butiama

Mwalimu na Mama Maria enzi hizo
Mwalimu na Mama Maria walipomtembelea mama mzazi wa Julius Kambarage Nyerere

Mwalimu akiingia kanisa la St. Peters. Alikuwa mcha Mungu sana
Mwalimu na Marais Kenneth Kaunda wa Zambia,
Mzee Jomo Kenyatta wa Kenya na Dr Milton Obote wa Uganda
Mwalimu akimkumbatia JK baada ya kukubali matokeo ya kura za kuwa mgombea urais wa CCM Mwaka 1995 huko Dodoma
Mwalimu akiongea na Mwandishi Freddy Macha walipokutana Rio de Janeiro, Brazil

Mwalimu na Mama Maria wakiwa India nyumbani
kwa Mama Indira Gandhi na mwanae Rajiv

Mwalimu akimkaribisha Madiba Ikulu, Dar

Mwalimu akitembea kuunga mkono Azimio la Arusha kwa kutembea toka Butiama Mwalimu, Mama Maria na Mzee John Malecela wakiwa na Iddi Amin, Uganda
Mwalimu akiwa na viongozi wengine wa nchi zisizofungamana na upande wowote
Mwalimu akitaniana na Tom Mboya na viongozi wengine Kenya

Mwalimu akisalimiana na Iddi Amin Dadah wakati wa mkutano wa OAU Addis Ababa, Ethiopia

Mwalimu na Mzee Malecela katika mkutano wa OAU ambapo Iddi Amini alikuwa akihutubia
Mwalimu akicheza bao na wazee wa Butiama huku Rais Ali Hassan Mwinyi na Mama Maria wakishuhudia
Mwalimu na Familia

Masikini Babu Seya!!

Sura ya mwisho ya babu seya na mwanae katika mahakama ya rufani

Image

HUKUMU ya Mahakama ya Rufaa, iliyotolewa na jopo la majaji watatu jana iliibua vilio na majonzi baada ya kumtia hatiani mwanamuziki maarufu nchini mwenye asili ya Kongo, Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na mwanaye Johnson Nguza hivyo kuendelea kutumikia kifungo cha maisha jela.

Hata hivyo, mahakama hiyo iliwaacha huru wanaye wengine wawili, Nguza Mbangu na Francis Nguza baada ya kubainika kuwa hawana hatia.

Babu Seya na wanaye, Johnson Nguza maarufu kama Papii Kocha, Nguza Mbangu na Francis Nguza walihukumiwa kifungo cha maisha mwaka 2004, baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwatia hatiani kwa makosa ya kubaka na kuwalawiti watoto wa kike waliokuwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Mashujaa jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo walikata rufaa Mahakama Kuu ambako Jaji Thomas Mihayo (mstaafu kwa sasa), aliwatia hatiani na kuunga mkono hukumu ya Hakimu Mkazi Mkuu, Addy Lyamuya; kisha wakakata rufaa katika Mahakama ya Rufaa.

Katika hukumu ya Mahakama ya Rufaa, iliyotolewa na jopo la majaji watatu, Salum Massati , Mbarouk Mbarouk, wakiongozwa na Jaji Nathalia Kimaro waliosikiliza rufaa hiyo, iliyosomwa jana na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa (DRCA), Neema Chusi, Babu Seya na mwanaye Papii Kocha walitiwa hatiani, huku Nguza Mbangu na Francis Nguza wakiachiwa huru.

Wakati akitoka nje ya mahakama kuelekea gerezani, Babu Seya aliendelea kusisitiza kuwa hakufanya kosa hilo na asingeweza kufanya hivyo na watoto wake, huku mwanaye Papii Kocha akisema kuwa wanategemea huruma ya Rais Kikwete na kwamba, wana imani kuwa atawatoa.

Wakili wao Mabere Marando alisema, "Tumeshinda nusu, tumeshindwa nusu. Huo ni uamuzi wa mahakama na kuwa hajawa na mpango wa kuendelea zaidi ya hapo."

Akisoma hukumu hiyo, Chusi alisema mahakama imeridhika na ushahidi ulioko kwenye kumbukumbu za mwenendo wa kesi hiyo kwa kila kosa na kwamba mrufani wa kwanza (Babu Seya) na wa pili (Papii Kocha), walihusika katika kutenda makosa na kwamba, utetezi wao kuwa hawakuwepo katike eneo la tukio ulikataliwa.

Kwa mujibu wa hukumu ya Mahakama ya Rufaa, Babu Seya alitiwa hatiani kwa makosa matano ya kubaka na Papii Kocha alitiwa hatiani kwa makosa mawili, wakati Mbangu na Francis hawakupatikana na hatia kwa makosa yote.

"Mrufani wa kwanza amepatikana na hatia ya makosa mawili ya ubakaji kosa la 7 na la 12 kinyume cha kifungu cha 130 (2)(e) na 131A vya Kanuni ya Adhabu (Penal Code) kama vilivyorekebishwa na vifungu vya 5 na 7 vya SOSPA (Sheria ya Makosa ya Kujamiiana),"ilisema hukumu hiyo na kuongeza:

Kwa kosa la 10 na 18 warufani namba moja (Babu Seya) na namba 2 (Papii Kocha) wamepatikana na hatia ya ubakaji kinyume cha kifungu cha 131A cha Kanuni ya Adhabu.

Hata hivyo katika kosa la 1,3,5,14, 20 na 22, warufani wote hawakupatikana na hatia, wakati katika kosa la 7 na 12 mrufani namba 1 mpaka namba 4 hawakupatikana na hatia huku kosa la 10 na 18 yakiwaondoa mrufani wa tatu (Mbangu) na wa nne (Francis).

“Hatimaye, hatia kwa mrufani namba tatu na wa nne inatanguliwa na hukumu pamoja na amri ya fidia inatupiliwa mbali. Wamewekwa huru isipokuwa kwa sababu nyingineyo. Na kwa mrufani wa kwanza na wa pili amri ya fidia bado inasimama tu kwa makosa ambayo yamewatia hatiani na inatupiliwa mbali kwa makosa yaliyobaki ambayo hayakuwatia hatiani,” ilisisitiza hukumu hiyo.

Mara baada ya Chusi kusoma hukumu hiyo majira ya saa 4:22 asubuhi, baadhi ya warufani hao waliangua kilio wakiwa kizimbani hususan Francis ambaye aliangua kilio kwa sauti kuu, huku Papii Kocha machozi yakimtiririka, lakini Babu Seya na Mbangu wakionekana kujawa na huzuni.

Chusi alianza kusoma hukumu hiyo kwa kuelezea kumbukumbu za mwenendo mzima wa kesi hiyo, akielezea ushahidi uliotolewa na mashahidi wa pande zote katika kesi ya msingi, hukumu ya rufaa ya kwanza ya Mahakama Kuu na hoja zilizotolewa na pande zote katika rufaa zote.

Kisha alisema; "Suala lililoko mbele yetu sasa ni kama ushahidi katika kumbukumbu ulithibitisha utendaji wa kosa. Kama ambavyo tayari imeshaonyeshwa PW 9 (Shahidi wa tisa wa upande wa mashtaka alikuwa ni mtoto wa miaka saba na alitoa ushahidi bila kiapo, ushahidi wake ulihitaji kuungwa mkono."

Katika ushahidi kwenye kumbukumbu hakuna mashaka kuwa PW9 alibakwa. Alithibitisha na kulikuwa na ushahidi wa PW20 kuwa PW9 alibakwa na PW9 alisema waomba rufaa ndio walimbaka.

Alisema jambo la msingi lilikuwa ni kuthibitsha kama waomba rufaa ndio walimbaka.

"Tumekwishatoa maoni juu ya mashahidi wa upande wa mashtaka na hatuhitaji kurudia kile ambacho tumekwishakisema. Inatosha kusema kwamba, kwenye kumbukumbu kuna ushahidi wa kutosha kuonyesha kuwa watoto walikuwa na uwezo wa kuingia katika nyumba ile bila kuonekana," alisema Chusi.

Alisema kwa mujibu wa uchunguzi wa hali ya nyumba iliyodaiwa kufanyika makosa yale kupitia kwa PW13, unaonyesha kuwa kulikuwa na mlango ambao ungeweza kutumiwa na watoto kuingia ndani ya nyumba ile namba 607 bila kuonekana.

Alisema kilichounga mkono ushahidi huo ni mazingira ya chumba cha mrufani wa kwanza (Babu Seya) ambamo ndimo kulimodaiwa kufanyiwa ubakaji, ambapo PW9 alieleza kuwa kuna godoro kitandani na godoro lingine ukutani na kwamba watoto wengine walikuwa wakilazwa kitandani na wengine kwenye godoro sakafuni.

"Tumesema mwanzoni mwa hukumu hii kuwa waathirika wa makosa ya ubakaji walikuwa ni watoto 10 na ushahidi wao katika maelezo yao kuhusu chumba cha mrufani wa kwanza unafanana,"alisema.

Akizungumzia utetezi wa Babu Seya kuwa alikuwa na matatizo ya nguvu za kiume na hivyo asingeweza kutenda kosa kama hilo na kwamba upande wa mashtaka ulikataa kwenda kumpima ili kuthibitishwa na daktari kama ana uwezo au hana uwezo wa kutenda kosa la ubakaji, mahakama iliutupilia mbali.

"Kwa maoni yetu upande wa mashtaka haukuwa na wajibu wa kufanya hivyo,"alisema Chusi katika hukumu hiyo na kuongeza:

"Tunasema hivyo kwa sababu katika kifungu cha 114 (1) cha Sheria ya Ushahidi (LEA) sura ya 6 kama ilivyorekebishwa mwaka 2002 suala la uwezo wa nguvu za kiume za mrufani ilikuwa katika ufahamu wake na suala la kuthibitisha lilikuwa juu yake kuthibitisha kuwa uume wake haukuwa ukifanya kazi".

Mahakama pia iliongeza kuwa ingawa kulikuwa na mazoezi katika nyumba hiyo(wanamuziki wa Bendi ya Akudo) haikuwa sababu ya kumzuia mrufani wa kwanza kutenda makosa kwa kuwa, kwa mujibu wa ushahidi matukio hayo yalikuwa yakifanyika kwa muda mfupi sana wakati wa mapumziko na wakati watoto hao wakitoka shule.

"Zaidi hakuna sababu kwa nini watoto wote hao waseme uongo dhidi yake na alikiri kuwa hakuwa na uhasama na mmoja wapo," iliongeza.

Kuhusu mrufani wa pili Papii Kocha, mahakama katika hukumu hiyo ilisema utetezi wake kuwa hakuwepo hauondoi uwezekano wa kutenda kosa.

"Tunasema hivyo kwa sababu kama ambavyo tumekwishaonyesha makosa yalikuwa yakitendeka kwa muda mfupi kama saa moja tu. Hii ina maana kwamba, hata kama mrufani wa pili alikuwa akifanya shughuli za kutumbuiza nje ya Dar es Salaam, lakini kuna wakati ambao alikuwa Dar es Salaam;

Kwa mujibu wa utetezi wake alikuwa akitoka nje ya Dar es Salaam kwa vipindi na si muda wote. Kwa namna hiyo hatuoni sababu yoyote PW8 ( mmoja wa watoto waathirika) kutengeneza ushahidi dhidi yake. Alikuwa ni mtoto mdogo ambaye hakujua hatari iliyokuwa mbele yake kwa kujihusisha katika, matendo ya ngono katika maisha yake".

Katika hukumu hiyo mahakama ilichambua ushahidi wa kila mtoto na kueleza jinsi ulivyoweza kuungwa mkono na mashahidi wengine, wakiwemo madaktari waliowafanyia vipimo baadhi ya watoto hao na kuthibitisha kuwa walikuwa wameingiliwa.

Ndugu na wakazi wa Dar es Salaam, wamepokea kwa mitazamo tofauti hukumu ya rufaa hiyo.

Akizungumza baada ya hukumu hiyo, Cheta Chinyama ambaye ni ndugu wa Babu Seya, alisema kuwa Mungu anajua kilichofanyika wao watabaki kumuomba ili aamue.

"Sina mengi ya kusema kwa kuwa Mungu ndiye anayejua yote yaliyofanyika, hivyo tunamuwachia yeye, kilichobaki tutamuomba Mungu ili aamue," alisema Chinyama kwa uchungu huku akilia kwa kwikwi.

Shangazi wa Babu Seya aliyejitambulisha kwa jina moja la Mwisa, alisema wao walitarajia kwamba ndugu zao wote wangeachiwa kwani walikuwa wakiomba sana kwa ajili yao.

Hata hivyo wanamuachia Mungu na kwamba wataendelea kusali kwa jina la Yesu ili siku moja waweze kuachiwa.

Mbali na masikitiko, baadhi ya wakazi wa jiji hilo wamedai kuwa pamoja na hukumu hiyo inaonyesha kuna siri kubwa imejificha ndani yake.

"Kitendo cha kuwaachia watuhumiwa wawili na kuendelea kuwafunga wengine inaonyesha kuna kitu kimetengenezwa kwa sababu kama walikuwa na hatia wote kwa nini leo wanawaachia wawili,"alihoji Kazimiri Pascal, mkazi wa Dar es Salaam.

Kwa upande wake Emmanuel Kashoke alisema maamuzi ya hukumu hiyo yameonyesha kasoro hasa katika vipimo vilivyodaiwa kuwatia hatiani watuhumiwa.

"Wanasema kwamba vipimo vya madaktari vilionyesha kuwa mlalamikaji alibakwa baada ya kupatikana na ugonjwa wa zinaa, sasa wamethibitisha vipi kama ule ugonjwa umesababishwa na mbakaji wakati hawakuchukua vipimo vya mbakaji, " alihoji Kashoke.

Salvatory Lumenyela, alizitaka nchi za Afrika kuanzisha mahakama ya rufaa ya Afrika kama ilivvyo kwa Ulaya ili kutoa fursa ya kupatikana kwa haki za wananchi.

"Lakini pia kuna haja kwa bara hili kuanzisha utaratibu wa kubadilishana wafungwa kwa sababu kama atakwenda nchini kwao anaweza kukata rufaa na kushinda kesi," alisema Lumenyela.

Yafuatayo ni maelezo zaidi juu ya hili

ILIO na majonzi jana vilitawala katika Mahakama ya Rufaa Tanzania jijini Dar es Salaam wakati mahakama hiyo ilipomuamuru mwanamuziki maarufu, Nguza Viking maarufu kwa jina la Babu Seya, na mwanawe, Papii Nguza (Papii Kocha) waendelee na vifungo vya maisha jela.

Kwa mujibu wa taratibu za mahakama Tanzania, uamuzi wa Mahakama ya Rufaa ni wa mwisho, hivyo Babu Seya na Papii Kocha watakaa jela maisha yao yote.

Mahakama hiyo imewaachia huru watoto wa Babu Seya, Nguza Mbangu na Francis Nguza.

Tangu Juni mwaka 2004 Babu Seya na wanawe watatu walikuwa jela kutumikia kifungo cha maisha kwa kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam iliona wana hatia ya kubaka ya kulawiti.

Kwa mujibu wa Mahakama ya Rufaa Tanzania, Babu Seya na Papii wamekutwa na hatia katika baadhi ya makosa, lakini Francis na Nguza Mbangu hawana hatia katika kosa lolote.

Baada ya Naibu Msajili wa mahakama hiyo, Neema Chusi, kusoma hukumu hiyo ya rufaa, watu walianza kulia, sauti ya Francis ilisikika zaidi pengine kutokana na uchungu wa kumuacha baba na kaka jela,sanjari na furaha ya kuachiwa huru.

Wakati Francis akiendelea kulia, watu wakiwemo waaandishi wa habari walimzunguka hivyo kusababisha wananchi wengine waliokuwa pembeni kulia, askari wakawa wanabubujikwa machozi.

Baada ya hukumu hiyo,wanamuziki hao walitolewa katika chumba cha mahakama na kupelekwa katika chumba kingine kilichozungukwa na watu wengi wakiwemo wasanii waliokwenda kusikiliza hukumu hiyo.

Wakati wakielekea katika chumba hicho Papii Kocha alisikika akisema “Kikwete atatusaidia, Kikwete atatusaidia”.

Chusi amesema, mahakama imeshindwa kuwatia hatiani Francis na Nguza Mbangu kwa sababu upande wa mashitaka umeshindwa kudhibitisha makosa dhidi yao.

Mahakama imetoa mfano kuwa, baadhi ya mashahidi waliopelekwa mahakamani na upande wa mashitaka waliweza kuwatambua Papii Kocha na Babu Seya lakini hawakuwatambua hao wengine hata kwa majina.

Awali Babu Seya na wanawe watatu walihukimiwa katika mashitaka 23, Mahakama ya Rufaa imeyaondoa mashitaka 11 ya kuingiliwa kinyume kwa maumbile kwa sababu hakuna mashitaka kama hayo chini ya sheria za kujamiiana.

Mahakama ilikubaliana na Wakili Mabere Marando kuwa ushahidi uliotolewa ulichukuliwa bila kiapo kwa vile hakimu hakujiridhisha kama watoto waliohusika walikuwa na uelewa wa kutambua kile walichokuwa wanakisema ni cha kweli na hivyo ushahidi huo ulitakiwa kuungwa mkono.

Mahakama hiyo imebaini kwamba,kulikuwa na ushahidi wa kutosha wa kuunga mkono ule wa watoto, ukiwemo unaoelezea namna chumba kilivyo ambacho kilikuwa kinatumika kwenye ubakaji na pia kitendo cha Babu Seya kuongeza sauti ya redio wakati wa kutenda kosa ili watu waliokuwa nje wasifahamu kilichokuwa kikiendelea ndani.

Juni 25, 2004, Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu, Hakimu Addy Lyamuya, aliwatia hatiani Babu Seya na wanawe watatu kwa makosa 23 ya ubakaji na ulawiti, akawahukumu kifungo cha maisha.

Wasanii hao walibainika kutenda makosa 10 ya kubaka watoto wenye umri kati ya miaka sita na minane na makosa mengine 11 ya kulawiti watoto wa kike wenye umri huo huo kati ya April na Oktoba 2003 katika maeneo ya Sinza kwa Remmy, Dar es Salaam.

Waliwasilisha rufaa kwenye jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa Tanzania akiwemo Mbarouk Salim, Salum Massati na Nathalia Kimaro.

Katika rufaa hiyo, wakili wa wasanii hao,Mabere Marando, alidai kuwa,Hakimu Lyamuya, aliingiza maslahi yake binafsi na hakuwa akizingatia ushahidi uliokuwa ukitolewa na upande wa washitakiwa.

Marando amedai kuwa, hakimu huyo alitoa kipaumbele kwa mashahidi wa upande wa Jamuhuri na kupuuza mashahidi wa upande wa washitakiwa hivyo kuwanyima haki.

Kwa mujibu wa Marando, watoto wote waliokwenda mahakamani kuthibitisha kwamba walibakwa au kulawitiwa na washitakiwa walitoa ushahidi bila kiapo isipokuwa mmoja kati ya 10 waliotoa ushahidi.

Amedai kwamba, watoto hao pia hawakurekodiwa ushahidi wao kabla ya kutoa ushahidi mahakamani jambo ambalo linakiuka sheria.

Marando amedai kuwa,baadhi ya watoto waliotoa ushahidi walikiri kutomtambua Babu Seya na washitakiwa wengine na kwamba, ripoti ya Daktari ilionyesha kwamba miongoni mwa watoto hao walikuwa ni bikira hivyo kumaanisha kwamba walikuwa hawakufanya kitendo chochote kilichohusiana na mashitaka hayo.




20 Years after Madiba release from prison

JUST FOR YOUR INFORMATION

At this stage everyone should be care,Girls are very attractive n men's are money makers.Gals concentrate on money and men's on on beauty,we are happy to visit Beaches,live shows,disco and rest in hotels but if we were wise enough we could visit ANGAZA, AMREF, WAMATA and CLINICS to update ourselves with status of HIV/AIDS so that we take precaution on how to use money and beauty.
JUST PROTECT YOURSELF YOU ARE AT RISK.
If you want to be happy never concern much with other people's minds